Friday , 9th Dec , 2016

Matayarisho ya tukio kubwa na kihistoria la utoaji tuzo kwa sanii wa muziki na filamu Afrika Mashariki yamekamilika, na kinachosubiriwa ni muda tu ufike, ili historia iandikwe.

Miongoni mwa watakaokabidhi tuzo kesho ni Tbway 360 kutoka 5Selekt ya EATV akiwa nyota wa Bongo Movie, Lulu

Tunaweza kusema kuwa kila kitu kiko 'mguu sawa' maana kila idara imejipanga kuanzia wasanii watakaoperfom, wasanii wanaowania tuzo, waratibu wa shughuli nzima, na wote watakaohusika kubwa ikiwa ni waandaaji wa ukumbi utakaotumiwa siku ya kesho.

Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha maandalizi ya ukumbi kwa siku ya leo ambao timu nzima ya wahusika ilikuwepo kufanya mazoezi (reheasal)

Stage katika hatua za mwisho za maandalizi

Host wa tukio hilo, Salama J, naye akiwa 'mguu sawa' kuandika historia

dancers katika maandalizi

Joachim Mabula - moja kati ya mashabiki wa EATv waliojipatia zawadi ya tiketi kuandika historia

Viti viko tayari kukaliwa, pia kuandika historia

Maeneo maalum ya kulia bata ndani ya ukumbi wa Mlimani City (juu na kulia) , kushoto ni maandalizi ya dancers

Baadhi ya wasanii wanaowania tuzo wakiwa ndani ya ukumbi

Wasanii wanaowania tuzo wakiitest stage

Kabla ya kuingia ndani, hili ni eneo maalum kwa ajili ya kujiselfisha na mastaa 

 

Bei ya tiketi ni Shilingi 20,000 kwa 50,000 endapo utanunua katika vituo vya mauzo lakini endapo utanunua kwa njia ya M Pesa, tiketi zinakuwa ni shilingi 18,000 na shilingi 45,000/-

 

 

Tags: