Monday , 3rd Aug , 2015

Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa, na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.

Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao

Defao ambaye hata hivyo haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka huko Kenya, kutokana na muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri kuyumba kisanaa na kiafya kwa msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa yake katika bara la Afrika na Ulaya.

Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.