Friday , 14th Mar , 2014

Msanii wa muziki C Pwaa, ametangaza ujio wake mpya akiwa chini ya usimamizi wa lebo mpya ya Brainstorm Music, akiwa na mpango mkubwa wa kubadilisha namna biashara ya muziki inavyokwenda sasa ili kumfaidisha kila msanii.

C Pwaa ambaye alituahidi hapo awali kuanza kutikisa mwaka 2014 kwa rekodi kali kuanzia mwezi huu, amesema kuwa akiwa na uongozi huu mpya, wakati wa kufanya rekodi kila kitu kitakuwa kinakwenda kwa makubaliano tofauti na mambo ambavyo yanakwenda katika industry hii kwa sasa.

C Pwaa amesema kuwa, hii ni hatua ya awali katika kuingiza biashara ya muziki hapa Tanzania katika mfumo ambao hutumika katika nchi nyingi ambazo zimeendelea ambazo amepata nafasi ya kuzitembelea.