Tuesday , 21st Jun , 2016

Msanii Chuchu Hans ametoa filamu inayoelezea mashariti ya kufuata katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, kuanzia muda wa wa kufuturu, kuandaa daku na jinsi ya kujistiri ndani ya mwenzi huo.

MOVE YA USIKU WA DAKU

Msanii wa kike kutoka katika kiwanda cha Bongo Move Chuchu Hans ameiambia eNewz kwamba ameamua kuandaa filamu hiyo amabayo itaonyesha masharti na utaratibu wa daku kwa watanzania wote bila kuangalia tofauti za dini zao.

Hata hivyo Chuchu amesema watu wengi huwa wanakuwa makini katika kufuatilia futari na mchana wanapokuwa wamefunga na muda wa kula daku, hivyo ameona ni vyema kuwakumbusha watu na kuwaonyesha umuhimu wa daku hasa katika mwenzi huu Mtukufu wa Ramadhani.