Thursday , 5th Feb , 2015

Chegge Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Saidi amesema kuwa kitendo cha wasanii kufanya kazi zao za muziki nje ya nchi kwa sasa, kitu ambacho baadhi ya wadau wanakitafsiri tofauti, ni kutokana na vile ambavyo soko na mashabiki wa muziki wanavyotaka.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chegge Chigunda

Chegge ambaye hivi karibuni amemaliza project yake kubwa kabisa inayokwenda kwa jina la 'Kaunyaka' akishirikiana na Temba huko Afrika Kusini, amesema kuwa hii ni katika kubadilisha ladha vilevile mazingira katika kuongezea nakshi katika kile wanachokifanya.