Monday , 9th Feb , 2015

Kutokana na hali ya maisha hususan kwa upande wa vijana kuendelea kuwa ngumu mitaani, Star wa muziki Chegge Chigunda amesema kuwa endapo mtu ana kipaji, nguvu ama elimu, si sawa kulalamika na kuishi katika hali ya umasikini.

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family Chegge Chigunda

Chegge amesema kwa kutumia nguvu, kipaji ama elimu maisha yanaweza kubadilika na mafanikio kupatikana, na kutoa wito kuwa kwa kijana aliyekamilika akiwa na sifa mojawapo kati ya hizi, kuishi chini ya dola moja kwa siku ni uzembe tu.