Sunday , 1st Jun , 2014

Msanii Jose Chameleone katika kuboresha kazi zake zote alizowahi kuzifanya katika muziki zikiwemo videos zake mbalimbali za muziki, mkali huyo ameweka wazi nia yake ya kurudia baadhi ya kazi zake hizo ili ziwe katika ubora zaidi.

Jose Chameleone akiwa amekaa chini katika pozi

Chameleone amesema kuwa anatarajia kutumia kitita cha pesa ambacho ni zaidi ya milioni 3 za Uganda kuzirudia video zake hizo zikiwemo ‘Tubonge’, ‘Badilisha’ na ‘Valu Valu’ ambazo ndizo zilizofanya vizuri katika chati mbalimbali Afrika Mashariki tokea zilipoachiwa hewani.

Mkali huyo ameongezea kuwa lengo zima la zoezi hili ni kuweka kazi zake zote ziweze kuwa katika ubora wa kimataifa na kuweza kuchezwa katika stesheni mbalimbali za luninga, ambapo kwa sasa mwimbaji huyo amepanga kushoot video zake upya katika mandhari tofauti nchini Afrika Kusini.