Sunday , 16th Mar , 2014

Kundi maarufu la muziki nchini Kenya (BMF) kwa kirefu Be My Faithful baada ya mafanikio waliyopata kupitia uzinduzi wa albamu yao hivi sasa wamerudi na project yao mpya iliyobatizwa jina ‘Highly Favoured'.

Project hiyo mpya kwa mwaka huu wa 2014 imemshirikisha msanii anayejulikana kwa jina little-known Mansura, akiwa ni mmoja wa wasanii watakoongezea ladha project hiyo inayotarajia kutoka hivi karibuni.

BMF hivi sasa wanaendelea kutikisa chati kupitia kazi yao iliyowapatia chati katika muziki inayokwenda kwa jina ‘I Live For You’, ambapo wamewasihi mashabiki Afrika Mashariki kutegemea kazi mpya kutoka kwao.