Meneja Masoko kutoka Benki ya Barclays Tanzania Joe Bendera (Kushoto) akijibu maswali ya wanafunzi wa UDSM, akiwa na washiriki wa EATV Awards Racheal Bithulo (Katikati) na Bright (Kulia)
Katika mafunzo hayo benki hiyo imewashirikisha wasanii wa muziki na filamu wanaowania Tuzo za EATV (EATV Awards) ikiwa kama moja ya wadhamini wake.
Meneja Masoko wa Barclays Bwana Joe Bendera amesema lengo la kufanya mafunzo hayo kwa wanafunzi ni kuwaweka tayari kwa ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao na kuwawezesha waanze sasa kufanya matayarisho ya kuingia kwenye soko la ajira badala ya kusubiri wamalize masomo ndipo waanze kuhangaikia ajira.
Amesema kupitia kampeni hiyo, Barclays itaendesha mafunzo maalum kwa makundi mbalimbali ya watu watakaohitaji, na kisha itawatunuku vyeti maalum vya kuhitimu vitakavyotambulika nchini Uingereza.
Mafunzo yakiendelea katika ukumbi wa Nyerere Theatre 1. UDSM
Amesema kampeni hiyo inaendeshwa katika nchi 10 barani Afrika, na watu watakaobahatika wataweza kupata fursa ya kutembelea katika nchi yoyote kati ya nchi hizo 10.
Akijibu maswali mbalimbali ya wanafunzi yaliyokuwa yakiulizwa katika mafunzo hayo leo, Bendera amesema mafunzo hayo yataendeshwa kwa njia mbili, moja ikiwa ni kupitia mtandao ( online) ambapo mtu atatakiwa kujisajili na kisha atapata mafunzo hayo.
Amesema njia nyingine itawahusu wanafunzi zaidi ambapo Barclays imeingia ubia na taasisi nyingine kuzungukia vyuo na taasisi mbalimba za elimu, na kutoa maelekezo zaidi ya kunufaika na mfunzo hayo.
Moja ya wanafunzi waliohudhuria, akiuliza swali
Katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ni ya maswali na majibu, mwanafunzi mmoja alitaka kujua endapo Benki hiyo inatoa ajira au kampeni yake ni ya mafunzo pekee ambapo Bendera alisema, kuwa benki hiyo ina programu ya kuajiri wanafunzi watakaokuwa tayari kupitia mpango huo kulingana na uhitaji lakini pia inafanya kazi ya kuwaunganisha wahitimu wenye ujuzi mbalimbali katika makampuni mengine .
"Sisi tuna connection na makampuni mengi, kwahiyo kupitia mpango huu, tutakuwa tukiwaunganisha na makampuni ambayo tuna ubia nayo kwa ajili ya ajira" Amesema Bendera.
Mwisho amewataka wanafunzi hao kujisajili sasa na kufungua milango ya ajira wakati watakapohitimu.
Baadhi ya washiriki wa EATV Awards wakijibu maswali
Mbali na ujumbe huo kutoka Barclays, washiriki wa EATV Awards waliofika katika mafunzo hayo wameelea uzoefu wao na njia walizopitia hadi kufikia mafanikio waliyonayo sasa na kupitia maswali yaliyoulizwa, wamewataka wanafunzi hao kutokata tamaa katika kila wajambo wanalofanya ili kufikia mafanikio.
Baadhi ya wasanii waliofika ni pamoja na Kajala Msanja, Daudi Michael, Lady Jay Dee, Feza Kessy, Shetta, Meya Shabani, Khadija Ally, Man Fizo, Racheal Bituro, Ruky Beiby. n.k
Tuzo za EATV zinafikia kilele chake Desemba 10 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam na zoezi la kupiga kura linafungwa Desemba 8. Tembelea eatv.tv/awards kwa taarifa zaidi pamoja na kupiga kura.
Joe Bendera - Meneja Masoko kutoka Barclays Bank