Friday , 30th Oct , 2015

Msanii Ben Pol amekuwa msanii wa kuigwa kwa kuwa kama balozi wa mkoa aliotoka Dodoma, kwa kuutangaza na kurudisha fadhila kwa mchango wake anaoupata kutokana na muziki.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio Ben Pol amesema anajivunia kuutangaza mkoa aliotoka, kwani pia anahamasisha uzalendo na watu kupenda kujivunia vya kwao.

"Mi nimekuwa mtu ambae niko proud kusema kama nimetokea Dodoma, na nimekuwa naitaja mara nyingi kwenye wimbo, kwenye interviews, najaribu kuhamasisha ule uzalendo au mtu kujivunia cha kwako", alisema Ben Pol.

Pia Ben Pol amesema mbali na hayo amekuwa akishiriki kwenye shughuli mbali mbali za maendeleo mkoani humo, pamoja na kutoa misaada mbali mbali.

"Lakini vile vile nimeshiriki uhamasishaji wa ujenzi wa maabara ambayo ilifanyika kama sikosei mwezi mei mwaka huu, ambayo ilisimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kwa hiyo nilishiriki, nilifanya perfomance, nilifanya uhamasishaji, na mpaka pesa ya ujenzi wa maabara kuu pale Dodoma ukawezekana kufanikiwa, nilifanya for free kwa sababu nilijua ni kazi ya kijamii, wakati mwengine hata charity", alisema Ben Pol.