Monday , 9th Nov , 2015

Nyota wa muziki Belle 9, licha ya mafanikio yake kimuziki kimataifa ambayo ndiyo yameanza kuonekana sasa, ameweka wazi kuwa tofauti na wengi wanavyofahamu, binafsi amekwishafanya maonesho mengi nje ya nchi.

Staa wa muziki Belle 9

Maonesho hayo yamempatia nafasi star huyo kujitangaza zaidi katika fani hiyo ikiwepo pia kushinda moja ya tuzo za heshima ya muziki nchini Ujerumani.

Belle 9 ambaye anabakia na rekodi ya kutowahi kuchukua tuzo hapa nchini, amesema kuwa tuzo hiyo ambayo aliishinda nje ya nchi, atawapatia mashabiki wake wote nafasi ya kuiona kwa mara ya kwanza kabisa katika project yake ya video inayofuata, ambayo hakutaka kuiweka wazi moja kwa moja.

Kuhusu kuwika kwake kimataifa na tuzo hiyo, Belle 9 anafunguka mwenyewe hapa.