msanii wa muziki wa dansi nchini Christian Bella
Christian Bella aka Mzee wa Masauti ameongea na enewz kuwa ameandaa tukio hilo kubwa la Live lililobatizwa jina 'Usiku wa Nani Kama Mama litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu, lengo kubwa la show hiyo ni ya kutoa heshima kubwa kwa akina mama ambao ndio watu muhimu katika jamii duniani.
Mfalme huyo wa masauti ameelezea kuwa show hiyo itakuwa ni Live ambapo mkali huyo amewashirikisha wasanii maarufu watakaomsindikiza stejini akiwemo Ommy Dimpoz aliyeshirikishwa katika wimbo huo, wengine watakaompa tafu live stejini ni wasanii Banana Zorro, Matonya, Cassim Mganga, Dully Sykes pamoja na bendi ya Malaika.