Wednesday , 10th Sep , 2014

Msanii wa muziki AY, ametangaza ujio wa kazi yake mpya ya kimataifa hivi karibuni, akiwa amemshirikisha msanii Miss Trinity pamoja na Lamyia.

msanii wa muziki nchini AY

Kazi hii itasimama kwa jina 'It's Going Down', mzigo mwingine matata kwaajili ya kuwarusha wapenda burudani.

Msanii huyu vilevile anatarajiwa kutoka na kazi ambayo amefanya na msanii wa kimataifa Sean Kingston, kazi ambayo inangojewa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wake ndani na nnje ya tanzania.