Thursday , 2nd Mar , 2017

Mwanamitindo Calisah ambaye ni moja ya watu ambao wanamsimamia rapa Young Killer amefunguka na kusema amembadilisha sana rapa huyo katika mambo mengi.

Mwanamitindo Calisah (kushoto), akiwa na Rapa Young Killer (katikati) wakati wakifanya video ya wimbo wa 'Sinaga swaga'

Miongoni mwa mambo anayodai kumbadilisha ni namna ambavyo anatakiwa kuvaa anapotoka na jinsi anavyotakiwa kuongea pindi anapokuwa na waandishi wa habari.

Mbali na hilo Calisah kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, anasema wimbo ambao utafuata kwa rapa huyo ni ule alioufanya na msanii Kaligraph kutokana nchini Kenya.

Msikilize hapa.....