Tuesday , 5th Sep , 2017

Rappa Fid Q ambaye anafanya vizuri kwenye hip hop ya bongo ametoa sababu iliyomfanya awachane wanafunzi wa vyuo wanaojiuza kwenye wimbo wa 'ulimi mbili', na kusema kwamba hakukusudia kufanya hivyo kwani wanachuo ndiyo watu waliomfikisha alipo sasa.

Fid Q

Akipiga stori kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Fid Q amesema aliandika wimbo huo baada ya kuona kwenye gazeti lililofanya utafiti suala hilo kwamba wanafunzi wa vyuo wanajiuza, lakini alishangazwa na habari hiyo kwani anapokutana nao hawafanani na matukio hayo.

Fid Q aliendelea kusema kwamba wanachuo ndiyo watu waliomsaidia kutengeneza 'brand' ya jina lake, na hata kama amewaimba humo haikuwa kwa nia mbaya.

Msikilize hapa chini.