Tuesday , 24th Jan , 2017

Msanii AT ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sili feel' amefunguka na kusema kuwa mwaka huu 2017 haitaji mchezo mchezo na kusema amejipanga vyema kuona anarudisha heshima yake na kukaa kileleni kabisa kwa kazi nzuri atakazo kuwa anaachia.

AT

AT akiongea na EATV, AT amedai kwa kuanzia mwisho wa mwezi huu au mwanzoni wa mwezi wa pili ataachia video ya wimbo wake huo 'Sili feel' na kusema baada ya hapo itakuwa ni bandika bandua.

"Nitaanza kutoa video ya kwanza mwisho wa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi wa pili, kisha baada ya hapo itakuwa ni bandika bandua maaana mwaka huu nitatoa video hata nane kama si kumi kabisa, maana nina kazi nyingi na ni kali hivyo nasema mwaka huu sitaki mchezo mchezo" alisema AT 

AT ambaye sasa amejichimbia jijini Mwanza kwa ajili ya kuendelea kurekodi kazi zake mbalimbali anasema ameamua kwenda kufanya kazi na maproducer wa mikoani na kusema kuwa wana vitu vizuri na uwezo mzuri ndiyo maana anawafuata huko huko kurekodi audio mbalimbali.