Friday , 11th Apr , 2014

Baada ya msanii Amani kufanya vizuri na ujio wake kupitia Ngoma ya Kiboko Changu
aliyowashirikisha wasanii Radio na Weasel kutoka Uganda na kutulia tena kwa muda, kwa sasa
mwanadada huyu amewaonyesha dalili za matumaini mashabiki zake.

R Kay, Amani

Amani ameanza mishe hizi baada ya kipindi cha mpito ambacho kiliambatana na misukosuko kutoka lebo ya Ogopa ambayo amekuwa akifanya nayo kazi, jambo ambalo lilizua wasiwasi juu ya muelekeo wa muziki wa mwanadada huyu.

Kwa sasa Amani anafanya kazi na mtayarishaji muziki R Kay, na hivi karibuni mashabiki wa
mwanadada huyu mkongwe katika muziki, wanatarajia ujio wa aina yake wa Amani kwa mwaka 2014

Tags: