Msanii wa bongofleva nchini Akil Ze Brain
Akili ameongea na eNewz kuwa kichupa hicho kipya kimefanyiwa kazi chini ya muongozaji mahiri Frank Obhthani kutoka Outcome Video Production, huku audio wa wimbo huo ukipikwa katika studio yake Akil iitwayo Akil Records.
Kichupa hicho ambacho kimefanyiwa upigaji picha Visiwani Zanzibar kitazinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza kesho Ijumaa usiku katika show yako bomba ya Friday Night Live ya EATV.