
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kalapina amesema alikuwa anapenda sana kucheza, lakini baada ya muziki wa rap kushika hatamu, alivutiwa na muziki huo, na kuamua mmoja wa wasanii wanaotangaza muziki huo.
"Kwanza kabisa brake dance ilianza kuja kabla ya rap music, mi mwenyewe nilikuwa brake dancer mmoja mkali tu DSM hapa, na nishawahi kupata ubingwa wa mkoa mwaka 1988, kwa hiyo rap music ilivyoanza kupiga hodi Pwani ya Afrika Mashariki, kiukweli makundi kama NWA, RUN DMC ndio waliniinspire sana nikawa napagawa sana, na alivyokuja kuibuka 2Pac miaka ya 91 92, 2Pac ndo akanipagawisha zaidi nikaona na mimi nahitaji kuwa artist", alisema Kalapina.
Kalapina ambaye kwa sasa anaendelea na muziki huo, pia amejikita kwenye harakati za kupambana na madawa ya kulevya kwa vijana, ili kuokoa kizazi pamoja na kutokomeza baishara hiyo haramu.
