Wednesday , 6th Jul , 2016

Ni zaidi ya mara moja msanii wa bongo fleva 20% kutangaza anarudi kombinenga kwa Man Wolter alaf

20% NA MAN WATER

Ni zaidi ya mara moja msanii wa bongo fleva 20% kutangaza anarudi kombinenga kwa Man Wolter alafu kazi hatuzioni zikifanyika ghafla tukaona kwenye mitandao Man kamrudisha 20% na kusaini mikataba kabisa enews ilitaka kujua kweli?.

Man wolter aliiambia Enews kuwa ni kweli kipindi hiki wamemrudisha 20% kombinenga rekodi na kipindi hiki wapo makini katika jambo wanalotaka kulifanya na tayari wanga ngoma zaidi ya tano ambazo zipo tayari kutoka.

Hata hivyo man water amesema imezoeleka kwa wasanii wengi kuimba nyimbo za mapenzi kwa kuwa zimezoeleka katika bongo fleva lakini kwa upande wa 20% yupo tofauti kwa kuwa nyimbo zake huwa na ujumbe katika jamii.

Hivyo mashabiki wasubirie ile ladha ya mashairi ya mapenzi ambayo waliyamisi katika mziki wabongo fleva kwa kile alichodai kuwa kwa sasa wasanii wengi hawatengenezi mziki mzuri wanatengeneza video zuri hivyo wananchi wategemee mziki mzuri kutoka kwa 20%.