Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kutolewa kwa hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwenda jela miezi mitano kutokana na kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.
"Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5. Wabunge wote wa vyama vya upinzani kwa namna moja ama nyingine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu", amesema Zitto.
Kwa upande mwingine, Zitto amedai anawasiliana na wenzake ili waweze kupata 'united Democratic Front'.





