
Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake akiwa na watoto wakimbizi
Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, katika ripoti yake iliyotolewa ikiangazia ongezeko la janga la wakimbizi na wahamiaji watoto.
Ripoti hiyo imesema idadi iliyosalia wanakimbia makwao kusaka maisha bora na usalama lakini wale wakiwa njiani wanakumbwa na majanga zaidi ikiwemo kuzama baharini, njaa, utapiamlo na hata usafirishaji haramu.
Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema wamependekeza mambo sita ikiwemo kulinda watoto wahamiaji na wakimbizi wanaosafiri wenyewe dhidi ya ghasia na ukatili, kuondoa uwekaji korokoroni watoto wanaosaka hifadhi na kuweka mbinu mbadala.