Thursday , 17th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika sekta ya mawasiliano hasa suala la uhalifu wa kutumia mtandao na imeahidi kwamba hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu itakua imetunga sheria tatu zitakazosimamia tatizo hilo.

Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar-es-salaam wakati alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo wenye lengo la kutathmini utendaji wa kazi kwa mwaka wa fedha 2014-2015.

Amesema chini ya sheria hiyo wizi kwa njia ya mitandao utaweza kudhibitiwa ingawa si kwa asilimia mia moja kwani wahalifu hao nao wana njia nyingi za kutumia kwa lengo la kutimiza matakwa yao.