Friday , 14th Dec , 2018

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu amesema kuwa rangi ya Njano kwenye bendera ya taifa itabaki kuwa ileile na sio rangi ya Dhahabu (Gold) kama ambavyo imeelekezwa kwenye taarifa ya wizara ya Mambo ya Ndani.

Bendera ya Tanzania.

Akizungumza kwenye East Africa BreakFast ya East Africa Radio, leo Disemba 14, Dkt. Semakafu amesema kuwa rangi hiyo ina maana yake kwenye bendera na haiwezi badilika kama ambavyo barua imezagaa mitandaoni inavyodai.

"Unajua hizi rangi zina maana na haiwezi kubadilika na ndio hali halisi, naomba muwe mnasikiliza vitu vinavyosemwa na waziri mwenye dhamana lakini hao wanaosemea mitandaoni inatakiwa watoe maelezo wenyewe", amesema Dkt. Semakafu.

Hayo yanajiri kukiwa na sintofahamu juu ya kusambaa kwa barua mitandaoni,  ambayo imeandikwa Novemba 23 mwaka huu ikiwa na kumbukumbu namba CHA-56/193/02/16, inasema wizara hiyo imepokea barua ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera na Nembo ya Taifa, na Wimbo wa Taifa.

Msikilize hapo chini, Dkt. Semakafu amefunguka zaidi.