Wednesday , 7th May , 2014

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema jumla ya wagonjwa 376 wameugua ugonjwa wa dengu Jijini Dar es Salaam kuanzia Januari hadi sasa ambapo miongoni mwao wawili wamefariki dunia.

Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, Dkt Seif Rashid.

Akiongea na East Africa Radio Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji Magonjwa wa wizara hiyo Dkt. Janet Mgamba amesema asilimia 80 kati ya waliopata maambukizi hayo ni wa kuanzia umri wa miaka 16 na kuendelea.

Dkt. Mgamba amesema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na mkakati wa kutoa elimu ya ugonjwa huo hadi kufikia katika ngazi chini ili kupunguza maambukizi yake.