Saturday , 22nd Sep , 2018

Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameongoza matembezi maalum kwa mamia ya wananchi wa jiji la Dar es salaam iliyolenga kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Matembezi hayo yalianzia eneo la viwanja vya mnazi majira ya saa 1 kamili na kuishia ukumbi wa karimjee saa 2 kamili asubuhi ambapo viongozi wa wizara akiwemo Mganga Mkuu wa Serikali na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali walishiriki.

Septemba 3 mwaka huu Waziri Ummy Mwalimu alisema  maambukizi ya virusi vya Ebola nchini yalyojitokeza nchini, lakini ni lazima Tanzania ichukue hatua ili kuhakikisha virusi vya Ebola havileti athari mbaya kama ilivyotokea kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo.

Miongoni mwa mikoa ambayo iko hatarini kukutwa na ugonjwa wa Ebola nchini ni ile iliyokaribu na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia na Kongo ni Mkoa wa Rukwa, Kagera, Katavi pamoja na Songea.