Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Taifa wa Chama hicho Bw. Roderick Lutembeka amesema kuahirisha kwa kikao hicho kunawapa hofu ya kushindwa kupatikana muafaka wa hali ya sintofahamu ya kisiasa inayoendelea nchini.
Aidha, Bw. Lutembeka amesema Chadema kinasubiri majibu yao kutoka kwa viongozi wa dini ambao waliwapa mapendekezo yao wayawasilishe kwa Rais katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu ya kisiasa