Tuesday , 2nd Aug , 2016

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA imewataka watuamiani wa bahari kuzingatia tahadhali na maelekezo yanayotolewa na mamlaka hiyo ili kuzuia majanga yasitokee.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imewataka watuamiani wa bahari kuzingatia tahadhali na maelekezo yanayotolewa na mamlaka hiyo ili kuzuia majanga yasitokee.

Akizungumza na East Africa Radio leo Meneja kitengo kikuu cha utabiri TMA Bwana Samweli Mbuya,amesema wanaendelea kufuatilia hali ya bahari kwa sasa na ikiwa kutatokea hatari yeyote katika bahari ofisi hiyo itatoa taarifa kwa haraka ili kuchukua hatua za haraka na tahadhari kwa watumiaji wa bahari.

Amesema hali ya hewa kwa sasa nchini ni majira ya kipupwe hivyo niwajibu wa kila mtu kuzingatia maelekezo ya mamlaka hiyo ili kupunguza majanga.

Amewataka watumiaji wa barabara hasa zile za mikoani ambazo zinaupepo wa wastani kuwa makini na ukungu ambao unatokea hasa nyakati za asubuhi kwani kwa kufanya hivyo wataepusha ajali na kuutolea mfano wa ajali ya gari la mafuta mkoani Morogoro ambayo ilisababishwa na dereva kushindwa kuona mbele kwa sababu ya kuwepo kwa ukungu