Meneja Mkuu wa Uendelevu wa Accacia, Assa Mwaipopo,
Akizungumza leo kwenye lango la Machame, akiwa na timu ya kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia, wakati wakijiandaa kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia watoto hao, Meneja Mkuu wa Uendelevu wa Acacia, Assa Mwaipopo, amesema timu hiyo ina watu 21 toka duniani.
Amesema wameamua kupanda mlima kama njia ya kuhamasisha watu mbalimbali kuchangia watoto wenye mazingira magumu, ili waweze kupata elimu kama watoto wengine.
Assa amesema mpango huo umesaidia sababu katika timu hiyo kuna watu toka Ufaransa, Uingereza, Marekani, Canada, Afrika Kusini, Kenya na Tanzania, ambao wamechanga dola za kimarekani 200,000 na kampuni yetu inatoa dola 200,000 na kuwa na jumla ya fedha sh. Milioni 800.
Amesema kwa kuanzia zitawasaidia watoto wengi na tayari kampuni yao imeanza mpango huo tangu mwaka 2010 na wanafunzi 158 wanaotoka maeneo ya Bulyanhulu wamenufaika na mwaka 2014 mpango ulipanuka na kunufaisha wanafunzi 5,000 wa maeneo ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara na wote wamefaulu vizuri.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, amesema tangu watangaze kwa njia mbalimbali juu ya lengo lao la kupamda mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha watu kuchangia elimu ya Tanzania, wamepata wahisani wengi waliounga mkono sula hilo.
Amesema wanaamini watoto wengi wakipata elimu wataweza kupata kazi hata kwenye migodi inayozunguka maeneo yao na kunufaika zaidi .