Friday , 21st Aug , 2015

Watanzania wamekumbushwa kuwa na namba za simu za kikosi cha zimamoto ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wakati pindi majanga ya moto yanapojitokeza kwenye maeneo yao ili yaweze kudhitiwa mapema.

Kikosi cha Zimamoto cha Faya kikiendeleza kuzima moto ulioenea kila pembe ya majengo

Wito huo umetolewa na afisa habari wa kikosi cha zima moto na uokoaji mkoani Mbeya Koplo Elivatho Mahangale alipokuwa akizungumza na East Africa radio.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawana namba za kikosi hicho hali inayopelekea kushindwa kutoa taarifa kwa wakati pindi janga la moto linapojitokeza.

Aidha amewataka wananchi kutumia namba ya dharura kwa makusudi yaliyokusudiwa na sio kutoa taarifa za uongo na kuonya kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.