Mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara Msafiri
Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 30.4.2013,wavamizi hao wapatao 115,walikubali kuondoka katika eneo hilo lakini mpaka sasa hawajatekeleza makubaliano hayo.
Shamba hilo lenye thamani ya milioni 800, hekari 16,000 limevamiwa na baadhi watu kutoka miji jirani ya wilaya hiyo na kuchukua hekari 450 kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kilimo bila idhini ya muwekezaji huyo.
Aidha kwa upande wa muwekezaji wa shamba hilo Rilash Kalaiya amesema kuwa bado wana uwezo wa kuliendeleza shamba hilo na kuiomba serikali kudumisha usalama wao ili kuweza kuendelea na shuguli za uzalishaji wa mazao kama awali.



