Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi.
Akizungumza mjini Dodoma leo, mwanasiasa huyo amesema kitendo cha kila mmoja kutangaza nia ya kugombea urais tena bila kufuata utaratibu ni jambo baya hususan kwa chama hicho na hakileti picha nzuri.
Mbali na Ndejembi amewataka wote wanaogombea urais kuondoa chuki baina yao na kuacha kupigana vijembe vya kuchafuana na kusema huo siyo ustaarabu.
Ndejembi amewataka watanzania kuwa wa moja huku akisema rais anayetakiwa ni mmoja tu na ndiye atakayepokea kijiti kutoka wa Rais Jakaya Kiwete .
Amesema,huyo mmoja atakayepatikana ndiye wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi wote wa Chama na Serikali watampigia kampeni za urais pindi wakati wa kufanya hivyo ukifika.
Hata hivyo Ndejembi amesema,kiongozi huyo atateuliwa kutokana na sifa zake za uongozi siyo ukabila wala nini bali anayefaa na kubarikiwa na Mwenyezi Mungu na kusema kuwa,mtu hapewi tu uongozi hivi hivi.