Wednesday , 1st Jun , 2016

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema Bungeni kwamba vijana wanaojiunga na jeshi la kujenga taifa asilimia 71% hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikali.

Mwinyi ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu aliyetaka kujua ni kwa nini serikali isiwahakikishie vijana wanaohitimu JKT kupata ajira kuliko kubaki na ujuzi wa kutumia silaha huku wengi wakiwa na vipaji mbalimbali.

Waziri Dkt. Mwinyi amesema kwamba wahitimu 71% hupata ajira na wengine hurudi makwao kutokana na uwezo wa serikali kuweza kuajiri vijana wote kw wakati mmoja.

Aidha Waziri amesema kwamba serikali itaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana watakaojiunga na JKT ili watakapo maliza waweze kupatiwa nyenzo za kujiajiri ili kuondokana na kusubiri ajira mtaani.