Thursday , 3rd Dec , 2015

Mhadhiri Chuo Kikuu cha Kilimo nchini Tanzania (SUA) ambaye ni mtaalamu wa chakula na lishe Prof. Joyce Kinabo amesema kuwa wananchi wa Tanzania bado wana uelewa mdogo wa masuala ya chakula na lishe hivyo kupelekea watu wengi kuugua magonjwa

yatokanayo na ukosefu wa baadhi ya madini mwilini.

Prof. Kinabo ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa kilimo, watumiaji na waagizaji wa chakua kutoka sekta za umma na watu binafsi kujadiliana jinsi ambavyo taasisi hizo zitaboresha usalama wa chakula na ulinzi kwa walaji na kuzitaka Mamlaka za Chakula na Dawa nchini (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango nchini (TBS) kuhakikisha wanasimamia ubora wa bidhaa ziingiazo nchini kwa kupita maeneo husika ambayo zinapita bidhaa hizo na zinapatikana kwa ajili ya matumizi.

Kwa upande wake Mhandisi wa Chakula kutoka chua cha SUA Prof. Bernard Chove ameitaka serikali kutumia tafiti zitolewazo na wataalamu nchini na kuzifanyia kazi sambamba na wadau na taasisi hizo watoe elimu yakutosha kuhusu vyakula...