Thursday , 4th Dec , 2014

Wananchi wa kijiji cha Kapunga katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya nchini Tanzania wameitaka serikali kutimiza ahadi yake ya kurejesha kwa wananchi hekta 1870 za ardhi ya kijiji ambazo wanadai kuwa zilichukuliwa na mwekezaji wa shamba hilo kimakosa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.

Wakizungumza kijijini hapo baadhi ya wananchi wamesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka alipofanya ziara na kuzungumza na wananchi hao alimtaka mwekezaji wa shamba hilo kuachia hecta 1870 za kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.

Ziara hiyo ilifanywa na Waziri ili kujiridhisha baada ya kupokea mgogoro huo kwa muda mrefu katika shamba hilo ambalo liliuzwa hekta 7370 badala ya 5500, na kwamba waziri huyo aliahidi kufikisha taarifa hizo haraka kwa Rais ili aweze kutenda haki kwa wananchi.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kapunga Bw. Ramadhani Ali Nyoni amesema baada ya kubinafsishwa kwa shamba hilo kuliwaongezea umasikini wananchi na wengine mpaka sasa wana hali ngumu ya maisha baada ya kukosa maeneo ya kulima.