Tuesday , 27th Sep , 2016

Wadau wa habari na waandishi wa habari kote nchini wametakiwa kutumia muda wa wiki tatu zilizobaki kikamilifu katika kuwasilisha maoni yao juu ya muswada wa sheria ya habari uliosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza.

Wanahabari wakiwa kazini

Mwitikio mdogo wa waandishi wa habari kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato wa muswada wa sheria ya huduma ya habari wa mwaka 2016 umewalazimu wadau wa habari kuwahimiza waandishi kupitia Club za Waandishi wa Habari Mikoani kutoa maoni yao juu ya mchakato huo.

Neville Meena na Theophil Makungu wote kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania amesema ni vyema wandishi wa habari wakajikita katika kuzingatia maslahi yao kwa kusoma na kufanya uchambuzi wa maudhui yaliyomo ndani ya muswada huo ili kupata sheria bora kwa tasnia yao.

"Muswada huu tusiwaachie wamiliki wa vyombo vya habari pekee tujitokeze na sisi kushiriki hatua zote kwani inahusu taaluma yetu kwa asilimia kubwa kwa hiyo kama walengwa ni vyema tukashiriki kikamilifu," alisema Meena.