Sunday , 24th Jul , 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amewataka wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini kujikita zaidi katika kusoma masomo ya Sayansi ili kuliongezea Taifa wataalamu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako

Akizungumza katika kilele cha maonyesho ya Teknolojia na Wanasayansi Vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Mtwara, amesema wizara yake itaongeza fursa nyingi katika masuala ya sayansi na teknolojia kwa kutambua mahitaji yaliyopo.

Mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa maonyesho hayo Dokta Gosbert Kamugisha, amesema vijana hao wako tayari kufanya masuala ya sayansi na teknolojia kwa masilahi ya Taifa, huku washindi wa kwanza na wa pili katika maonyesho hayo kutoka shule za Mtwara Ufundi na Mtwara Wasichana wakielezea furaha zao baada ya kutangazwa washindi.

Sauti ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,