Thursday , 26th Jun , 2014

Umoja wa wamiliki wa shuke na vyuo binafsi nchini Tanzania TAMONGSCO umesema kwamba uko tayari kupunguza ada ya shule kwa asilimia 30 ikiwa serikali itafuta kodi ambayo shule na vyuo hivyo vinalipa.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa.

Katibu mkuu wa TAMONGSCO Benjamin Nkonya amesema kwamba wamuiliki wa shule na vyo binafsi nchini walikutana na kamati ya bunge ya bajeti na kamishna wa mamlaka ya kodi ya mapato TRA mjini Dodoma na kuanisha matakwa yao.

Nkonya amesema sera ya elimu inataka kila shule iliyosajiliwa inatakiwa kutoa elimu kama huduma na siyo kujinufaisha kwa faida laki hata hivyo shule hizo zinalazimika kulipa aina ya kodi kumi.