Monday , 18th Jul , 2016

Miezi sita baada ya sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne hapa nchini waalimu wamebaini changamoto mbalimbali ambapo wanaomba serikali kuzishugulikia ili elimu bora itolewa kwa wanafunzi wengi walio jitokeza kupata elimu.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na waandishi.

Baada ya sera hiyo kuanza wanafunzi wengi wamejitokeza kupata elimu, huku changamoto ya awali ya uchache wa madawati imetatuliwa tayari sasa wanafuzi wanakaa kwenye madawati lakini shida inakuja katika suala ya vyumba vya madarasa.

Waalimu mkoani Njombe pamoja na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakaa katika madawati wamemuomba Rais kutatua tatizo la uchache wa waalimu, vitendea kazi pamoja na madarasa kwa baadhi ya shule.

Tatizo hili linaenda sambamba na uhitaji wa vitendea kazi kwa waalimu wanao fundisha watoto wenye uhitaji maalumu kama wale wenye uoni hafifu.

Viongozi wa chama cha waalimu CWT mkoa wa Njombe wanaona umuhimu wa kutoa elimu kwa waalimu wanawake na walemavu huku wakiwaelimisha juu ya sera ya elimu bure.

Sauti ya Sherida Mtaki, mwenyekiti CWT wanawake taifa