Tuesday , 17th Mar , 2015

Chama cha wa walimu na kampuni ya walimu nchini wanataanza kuuza hisa kwa ajili yakukusanya Mtaji ili kuanzisha Benki ya Walimu nchini ambayo itawasaidia walimu pamoja na watanzania kwa ujumla.

Akizungumza jana Jijini Dar es salaam Rais wa Chama cha Walimu nchini Gratian Mukoba amesema hisa hizo zitaanza kuuzwa Jumatatu wiki ijayo katika Soko la hisa la Dar es salaam wiki ijayo pamoja na Mawakala wengine ikiwemo mabenki.

Kwa Upande wake Meneja Mradi wa Uanzishaji wa Benki hiyo Ronald Manongi amesema mpaka sasa wanamtaji wa Shiling billioni17 huku Mtaji wa chini kabisa kwa mujibu wa Benki kuu ni Bilion 15,

Manongi ameongeza kuwa wanataka kuwafikia watu laki tano huku kila hisa itauzwa shiling elfu moja huku Walimu pekee wakiwa ni laki mbili.

Benki hiyo itawahudumia Watu wote bila kujali kama ni Waalimu au wananchi wa kawaida,