Wednesday , 5th Aug , 2015

Serikali ya Tanzania hatimaye imeanzisha rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo itakuwa na juk

Serikali ya Tanzania hatimaye imeanzisha rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo itakuwa na jukumu la kutoa mikopo nafuu kwa ajili ya miradi yote ya kilimo na ambayo mikopo yake haiwezi kupatikana katika benki za kawaida za biashara.

Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Bw. Thomas Samkyi, amesema kuwa benki hiyo itazinduliwa rasmi na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati wa sherehe za Nane Nane zitakazofanyika kitaifa mkoani Lindi, ili kutoa fursa kwa wakulima kufahamu fursa hiyo mpya ya mikopo kwa ajili ya miradi ya kilimo.

Samkyi amefafanua kuwa tofauti na benki nyingine, benki hiyo itakuwa inatoa mikopo ya muda mrefu na inayokidhi mahitaji ya sekta ya kilimo, hatua aliyodai itasaidia kukuza sekta ya kilimo, ili kutimiza dhana ya kilimo kwanza inayolenga kugeuza kilimo toka kuwa cha chakula na kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara.