Monday , 4th May , 2015

Serikali wilayani Njombe imesema kuwa imefanya jitihada zake nyingi za kuhakikisha wananchi wanao jihusisha na kilimo cha matunda na mbogamboga wanapata masoko ya uhakika kwa mazao yao yaliyo sindikwa ndani na nje ya nchi.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akiongea na wadau Mkoani humo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi ya kutoa elimu ya kusindika mboga za majani na matunda ya kijani kibichi Tanzania, mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba amesema kuwa amekuwa akitafuta mbinu mbalimbali za kuwainua kiuchumi wakulima wa mbogamboga na matunda mkoa wa Njombe.

Amesema kuwa amekuwa akipambana kila kukicha kuhakikisha wakulima hao wanakuwa na masoko ya uhakika wa mazao yao ya mbogamboga na matunda ambapo wakulima wengi mazao yao yamekuwa yakipotelea shambani.

Amesema kutokana na wakulima kutokuwa na elimu ya ujasiliamali wamekuwa wakishinda kushusha bei ili apate angalau faida kidogo anaona bora matunda yakaharibika.

Amesema kuwa kuja kwa taasisi ya kijani kibichi kutasaidia kuinua uchumi wa wakulima wa mbogamboga na wakina mama ambao wamekuwa wakipigana kutokana na kilimo.

Aidha Dumba amesema kuwa hata wana wa Israel walipo kuwa jangwani Mungu aliwapa chakula lakini alitaka wafanyakazi kwa kukusanya chakula na kuwa aliwapa chakula lakini hakuwapelekea hadi ndani na kuwataka wakulima kuacha uvivu wa kujifunza mbinu mbalimbali za kujiongezea kipato.

Kwa upande wa taasisi hiyo imesema kuwa itajikita hufundisha uzalishaji wa kisasa na usindikaji wa mazao mabichi kama mboga za majani, nyanya na matunda mengine.