Wednesday , 13th Jul , 2016

Utafiti katika mgodi wa dhahabu wa Nyanzaga Mkoani Mwanza, unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 30 kuthibitisha kiwango cha dhahabu iliypo na kutoa mwelekeo wa uchimbaji wa madini hayo.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. William Ngeleja, akiongea na Wananchi wa Jimbo lake

Akiwa katika ziara ya kikazi ya kuongea na wananchi wilayani Sengerema mbunge wa jimbo hilo Mhe. William Ngeleja, amesema mafaniko ya mgodi wa Nyanzaga yanategemea mahusiano mazuri kati ya mwekezaji na wananchi.

Mhe Ngeleja amesema endapo mgodi huo utatekeleza majukumu yake kwa wananchi itasaidia kwa kiwango kikubwa kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo na taifa kwa ujumla kwa kuboresha huduma za kijamii.

Mhe Ngeleja ameongeza kuwa wanatarajia mgodi huo kutoa fursa za ajira kwa wakazi wengi wa eneo hilo la mgodi kuchangia pato la taifa kwa kulipa kama inavyotakiwa ili wakazi wa eneo hilo na Taifa kwa ujumla lipate maendeleo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. William Ngeleja