Thursday , 4th Aug , 2016

Wagunduzi nchini Tanzania wametakiwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kubuni na kugundua teknolojia mpya zitakazosaidia kutatua matatizo ya jamii pamoja na kukuza uchumi wa viwanda .

Mkurugenzi wa Mawasiliano wizara ya Mawasiliano,Ujenzi na Mawasiliano Clarence Ichwekeleza

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wizara ya Mawasiliano,Ujenzi na Mawasiliano Clarence Ichwekeleza, amesema kuwa kupitia mradi wa Tanza Ict umewasaidia wabunifu na wagunduzi kugundua teknolojia mpya zitakazoisaidia jamiii katika masuala ya nishati na kuweka mazingira safi.

Mkurugenzi wa Shirika la TEMDO Kalutu Koshuma amesema kuwa TEHAMA imewasaidia wagunduzi Kupata taarifa muhimu mbalimbali za wagunduzi wengine katika nchi mbalimbali ili ubunifu wao uweze kufanikiwa na usijirudie

Mbunifu wa Teknolojia ya kutumia taka za mjini kutengeneza Mkaa Adam Mfaraji amesema kuwa fedha walizopata kupitia mradi wa Tanz Ict imewasaidia kubuni mashine ya kubadili taka za mjini kuwa mkao unaotumika kama nishati mbadala mradi ambao unatarajia kwenda sokoni na kuwanufaisha kiuchumi.

Ubunifu ni nyezo muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda kama ilivyo adhama ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano John Pombe Magufuli

Mkurugenzi wa Mawasiliano wizara ya Mawasiliano,Ujenzi na Mawasiliano Clarence Ichwekeleza