Tuesday , 14th Jul , 2015

Wadau mbalimbali wametoa maoni ya juu ya matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi kwa kuuawa na kuibiwa silaha huku wakieleza kuwa polisi inatakiwa kutafatakari upya katika dhana nzima ya ulinzi shirikishi.

Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Dk, Benson Bana.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Dk, Benson Bana amesema dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi itafakariwe upya na kupewa msukumo pia askari wawe wakali kwa kutambua sio kila raia ni mwema.

Amesema kuwa jeshi lina wataalamu wengi na linahitaji nguvu ya pomoja kati ya raia na vyombo vyenye dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zao kufanikisha ulinzi nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa amesema inaonesha serikali haikuwa makini juu ya suala hilo kwa kuwa sio mara ya kwanza kutokea kwa matukio hayo.