Mkuu wa Wilaya ya Ilala Jijini, Dar es Salaam, Raymond Mushi,
Mushi amesema hayo jana wakati akipokea msaada wa fedha ya zaidi ya shilingi milioni 7 kutoka kwa shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC),kwa ajili ya kununulia madawati ya shule ya msingi Zimbili iliyopo eneo la Kinyerezi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa bado kuna uhitaji wa madawati karibu Elfu 16,ili kumaliza changamoto hiyo katika shule za masingi wilayani ilala ambapo kwa eneo la Segerea ni shule nne tu ambazo zimebaki na changamoto ya madawati.
Kwa upande wake Meneja mawasiliano wa TPDC,Maria Mselemo, amesema kuwa shirika hilo linaendelea na mkakati wake wa utoleaji wa huduma za kijamii ili kuunga mkono jitihada za rais Dkt. John Maguguli, katika kuwahudumia wananchi.
Amesema kuwa shirika hilo litakuwa linatoa misaada katika maeneo yote nchini wala sio katika maeneo yaliyopitiwa na mradi wa gesi peke yake hivyo watakua wanasaidia kuchimba visima, Ujenzi wa Madarasa, madawati na na shughuli nyingine za kijamii.