
Wakichangia katika siku ya pili ya kujadili hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2015, mpango wa maendeleo pamoja na bajeti ya mwaka 2016/2017 baadhi ya wabunge waliochangia mjadala huo walianza kwa kutaka kodi ya kiinua mgongo ifanywe kwa wote na sio wabunge pekee.
Wakielezea kuhusu athari zinazotokana na kupandisha kodi ya mitumba wabunge hao wametaka serikali kupitia upya pendekezo hilo kwani litakuwa na athari kubwa kwa wananchi ambao wengi wao bado wanatumia mitumba na serikali haikuwekeza vya kutosha kuwapatia wananchi nguo.
Aidha wabunge hao wamehoji pesa kidogo anazopewa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) katika shughuli zake na kutaka serikali itazame upya tena bajeti ya CAG.