
Rais wa Jukwaa wa waangalizi kutoka nchi za maziwa makuu Seneta Peter Mositet ..
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Jukwaa wa waangalizi kutoka nchi za maziwa makuu Seneta Peter Mositet na kuongeza kuwa wapo nchini kwa kuangalia namna kampeni zinavofanywa.
Aidha Mh. Mosteti ameongeza kuwa pia watafatilia sheria za uchaguzi mkuu kama zinafuatwa siku ya kupiga kura mpaka utangazaji wa matokeo ambapo watatoa tathimini yao kuhusu uhalali wa uchaguzi huo.
Seneta Mosteti amesema anaamini Tanzania ni nchi ya amani na watadumisha amani na uchaguzi utafanyika kwa utulivu mpaka siku yatakapotajwa matokeo na hatimaye kufikia makubaliano ya ushindi utakaopatikana.