Saturday , 25th Jun , 2016

Waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika kusaidia kukomesha madhila yanayowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi Ikpnoswa Ero

Hayo yamesemwa na Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi Ikpnoswa Ero.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kongamano la kwanza la mataifa ya Afrika kuhusu ulemavu wa ngozi wiki hii, amesema vyombo vya habari ni kioo cha jamii na wanawajibu mkubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klub za waandishi wa habari nchini, Abubakar Karsan, amesema kuwa waandishi wa habari hawana budi kuongeza jitihada zaidi kufichua matukio hayo ya uhalifu ili yaweze kudhibitiwa na kutokomezwa kabisa.