Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala
Hayo yamesemwa na Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa kumbukizi ya kuwaenzi wataalum wa masuala ya lugha ya kiswahili waliofariki dunia huku akisema ni vyema wataalamu hao wakaenziwa kwa kuyatunza na kuyatumia machapisho yaliokwisha andikwa kwa maendeleo ya kiswahili.
Nao baadhi ya washiriki kutoka idara mbalimbali zinazoshughulika na lugha ya kiswahili akiwemo mkurugenzi msaidizi wa lugha kutoka wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Dkt..Hajjat Kitogo amesema majarida ya kitaalum ni muhumi na hivyo watu wajijengee utamaduni wa kuyasoma.
Miongoni mwa watu wanakumbukwa kwa mchango wao katika taaluma ya kiswahili ni Profesa Yareld Kihore Profesa.Eliezer Chiduo, mwalimu Gordian Katikiro na mwalimu Edwin Semezaba wote wakiwa ni watunzi wa vitabu na majarida mbalimbali ya lugha ya kiswahili.